Topic outline
Utangulizi
Karibu kwenye kozi hii ya BBC Media Action, Kuripoti Mabadiliko ya Tabianchi. Ni Furaha kwetu wewe kujiunga nasi.
Kozi hii itakusaidia kuelewa sayansi inayochangia sababu za mabadiliko ya hali ya hewa,
jinsi mashirika na jumuiya za kimataifa zinavyoitikia na jinsi wewe kama
mwanahabari unavyoweza kuiandika vyema kwa hadhira yako.
Kuwasiliana kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ni muhimu sana kwani ongezeko la matukio
ya hali ya hewa kali yana madhara makubwa kwa jamii maskini zaidi katika eneo hilo.
Kutoa hadithi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kunaweza kusaidia kuboresha
uelewa wa hadhira na kuwapa maarifa na ujuzi unaohitajika ili kuwasaidia kukabiliana na hali.
Moduli ziko wazi kwa umma.